#HABARI: Wajasiriamali mkoani Manyara, wataanza kunufaika na mashine za kisasa za kuongeza thamani ya mazao ya nafaka, ikiwemo alizeti ili waweze kuzalisha bidhaa bora wa kitaifa na kimataifa pamoja na kupata uhakika wa masoko.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Bi. Queen Sendiga, akizungumza na wanahabari amesema kuwa mkoa huo unatarajiwa kufanya maonyesho ya wajasiriamali ya Tanzanite Manyara Trade Fair Octoba 20 mpaka 30 mwaka 2024, viwanjavya Tanzanite Kwaraa mkoani humo, ambapo teknolojia za kuongeza thamani ya mazao zitaonyeshwa na jinsi zinavyofanya kazi.