#HABARI: Viongozi na waumini wa dini dhehebu la Mashahidi wa Jehova, mkoani Kilimanjaro, wameungana na madhehebu mengine nchini pamoja na watanzania kupinga vitendo vya utekaji wa watoto, ulawiti pamoja na unyanyasaji wa kijinsia ambavyo vinatajwa kuongezeka katika jamii kinyume na maadili ya kitanzania
Wametoa kauli hiyo katika kusanyiko lilikwakutanisha waumini hao pamoja na viongozi wadini kutoka katika dhehebu hilo kusanyiko lijukanalo kama tangaza habari njema ambao wamekutana katika Manispaa ya moshi.