#HABARI: Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Songwe, kupitia kwa Mwenyekiti wao Bi. Fatuma Hassan, amekemea kukithiri kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia mkoani humo ikiwemo ulawiti, ubakaji na mimba za utotoni, ambazo zimekuwa chanzo cha wanafunzi wengi wa kike kukatisha masomo.
Akizungumza na vijana wanaounda umoja huo kutoka Wilaya zote nne za mkoa huo waliokutana kujadili mambo mbalimbali ikiwemo kuweka mikakati kuelekea chaguzi zijazo, Bi. Fatuma, amewataka vijana hao kuwa watetezi na walinzi hasa kwa mabinti ambao ni wanafunzi, huku akiomba serikali kuwawajibisha viongozi wa umoja huo ambao maeneo yao yatabainika kuwepo kwa vitendo hivyo.