#HABARI: Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) imefanikiwa kukamilisha utafiti na usajili wa aina tano za mbegu za mali…

#HABARI: Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) imefanikiwa kukamilisha utafiti na usajili wa aina tano za mbegu za malisho ya mifugo zitakazosaidia kurahisisha upatikanaji wa malisho ya mifugo jambo ambalo litasaidia kumaliza migogoro kati ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi.

Mbegu hizo ni pamoja na _Cenchrus ciliaris_ (TALIRICENCH 1), _Medicago sativa _(TALIRIALFA 1), _Desmodium intortum_ (TALIRIDESMO 1), _Macroptilium atropurpureum_ (TALIRIMACRO 1) na _Chloris gayana_ (TALIRICHLO 1) ambapo mkakati wa Taasisi hiyo ni kuzizalisha kwa wingi na kuzisambaza kwenye maduka ya pembejeo za kilimo.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo Prof. Erick Vitus Komba maonesho ya 31 ya Kilimo ya Kimataifa (Nanenane) viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma , na kwamba kwa mujibu wa sheria, kanuni na miongozo ya uzalishaji wa mbegu chini ya kifungu cha 21 cha sheria ya mbegu Na. 18 ya mwaka 2003 na marekebisho yake ya mwaka 2014 Serikali imeidhinisha matumizi ya mbegu hizo.