#HABARI: Shuguli za kibinadamu zitokanazo na baadhi ya wananchi kukata miti na kuchoma mkaa, zimesababisha uharibifu wa mazingira, wilayani Mkalama, mkoani Singida, jambo ambalo limesababisha baadhi ya maeneo kukosa mvua na kupelekea mabadiliko ya tabia ya nchi.
Hayo yamebainika kwenye mpango wa kujadili jinsi ya kupanga mkakati wa uhifadhi wa mazingira ulioandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Helvertas, kupitia mradi wa kijani hai na uhifadhi wa mazingira Wilaya ya Mkalama.