#HABARI: Shehena ya vipodozi vyenye viambata sumu, iliyokuwa ikiingizwa nchini kimagendo ikitokea nchi jirani kupitia mpaka wa Tunduma, imeteketezwa mkoani Mbeya, baada ya kukamatwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja.
Meneja Msaidizi wa Forodha mkoa wa Mbeya, Bw.Nsajigwa Mwambegele ,anaeleza mbinu ambazo wafanyabiashara wasio waaminifu wavyozitumia kuingiza vipodozi hivyo nchini.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania