#HABARI: Shalom Albert Tarimo (21), Mkazi wa Msaranga, Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, amefariki dunia baada ya kutumbuki…

#HABARI: Shalom Albert Tarimo (21), Mkazi wa Msaranga, Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, amefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye kisima kilichokuwa kikitumika kuhifadhia mafuta ya Dizeli lita 40,000 katika moja ya kituo cha mafuta kilichopo katikati ya mji wa Moshi.

Shalom alikuwa akifanya kazi binafsi za usafishaji wa kisima katika kituo hicho cha kuhifadhia mafuta ya Dizeli ambacho jina ‘Kapuni’ kwenye Manispaa ya Moshi.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mwili umepelekwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mawenzi.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow @radioonetanzania