#HABARI: Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekubaliana kushirikiana na Chuo cha Mafunzo ya Mapishi cha Basque (Basque…

#HABARI: Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekubaliana kushirikiana na Chuo cha Mafunzo ya Mapishi cha Basque (Basque Culinary Center) cha nchini Uhispania kilichojikita katika kutoa mafunzo, kufanya tafiti, ubunifu na kufanya uendelezaji wa utalii wa vyakula (Gastronimy Tourism) na lishe.

Hayo yamebainika katika kikao kati ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) na Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha Mafunzo cha Basque, Joxe Mari Aizega wakati wa ziara ya kutembelea Kijiji cha Utamaduni cha Umuzi kilichopo jijini Victoria Falls nchini Zimbabwe iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UN Tourism).

Lengo la kushirikiana na chuo hicho kinachoongoza duniani kwa Sayansi ya Utalii wa Vyakula, Utafiti na Ubunifu ni kukuza Utalii wa Vyakula nchini Tanzania.