#HABARI: Serikali nchini Burundi, imeweka mpango wa kitaifa wa kukabiliana na janga la ugonjwa wa homa ya Nyani, baada ya kuripo…

#HABARI: Serikali nchini Burundi, imeweka mpango wa kitaifa wa kukabiliana na janga la ugonjwa wa homa ya Nyani, baada ya kuripotiwa visa vya mambukizi ya ugonjwa huo kwenye Wilaya 49 za afya na Wilaya 22 nchini humo.

Mpango mkakati huo umebainishwa na Waziri wa Afya nchini humo, Dkt.Lydwine Baradahana, ambapo amesema kutokana na bei ya matibabu kuwa kubwa, serikali imechukuwa uamuzi wa kutoa matibabu bure kwa wagonjwa wa homa ya nyani nchini humo.

Ni siku zaidi ya 15 tangu kuripotiwe kesi ya ugonjwa wa homa ya Nyani, ambapo serikali imeweka mpango ndani ya miezi sita kupambana na homa ya Nyani.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow @radioonetanzania