#HABARI: Serikali imesema kuwa mradi mkubwa wa usafirishaji umeme wa TAZA, unaohusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa m…

#HABARI: Serikali imesema kuwa mradi mkubwa wa usafirishaji umeme wa TAZA, unaohusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 400, kutoka Iringa hadi Sumbawanga na kuunganisha Tanzania na Zambia (TAZA), pamoja na vituo vya kupoza umeme vya Tagamenda, Kisada, Iganjo, Nkengamo na Malangali utawezesha kuunganisha Bara la Afrika kwa nishati ya umeme kutoka Afrika Kusini hadi Ethiopia.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko wakati akiweka jiwe la msingi la utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa usafirishaji umeme ambao unahusisha kipande cha kilomita 4 kutoka Tunduma hadi Nakonde mpakani mwa Tanzania na Zambia.

“ Kwa kutambua kuwa nishati ni kichocheo cha uchumi, Serikali imeendelea kutekekeza miradi mbalimbali ukiwemo wa Julius Nyerere (JNHPP), ambao tayari unaingiza megawati 705 kwenye gridi ya Taifa na hivyo kuwezesha nchi kuwa na ziada ya umeme, huku mtambo mwingine wa megawati 235 ukitarajiwa kuwashwa mwezi Agosti” Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko.