#HABARI: Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi, amesema katika utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2020 hadi 2025 , Serikali imedhamiria kusimamia ubora wa bidhaa kwa kuziweshesha taasisi zinazosimamia ubora, ikiwemo Taasisi ya viwango Zanzibar (ZBS) kwa kuwa na maabara za kisasa na wataalamu wenye uwezo kwa kazi upimaji na ukaguzi.
Dkt.Mwinyi amebainisha hayo leo, alipofungua kituo cha ukaguzi wa vyombo vya moto, Maruhubi Mkoa wa Mjini Magharibi na kusisitiza kuwa serikali imeendelea kuchukua hatua ya kuimarisha miundombinu ya ZBS kwa kujenga kituo cha ukaguzi wa vyombo vya moto ambacho amekifungua.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania