#HABARI: Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema serikali itaendelea kutoa vibali vya ajira kwa kila mwaka katika Sekta ya Afya, ili kupunguza changamoto ya uhaba wa watumishi kutokana na maendeleo katika sekta hiyo.
Rais Dkt. Samia, amesema hayo wakati akifunga Kongamano la Kumbukizi la Hayati Benjamini Mkapa, ambalo limewakutanisha wadau wa maendeleo katika Sekta ya Afya kutoka ndani na nje ya nchi, kujadili changamoto na namna ya kuzitatua katika upande wa rasilimali watu.
“Changamoto ya upungufu wa watumishi katika Sekta ya Afya inatokana na kukua kwa idadi ya watu ambapo inapelekea kuongezeka uhitaji wa wataalamu wa afya na walimu, lakini endapo Tanzania itakua kiuchumi changamoto hiyo itaondoka.” Rais Samia.