#HABARI: Rais wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, amewaomba Wakazi wa Ukonga kumshika Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Jerry Silaa kwakuwa ni Waziri anayefanya kazi vizuri.
“Nawashukuru Wakazi wa Ukonga mmenipa Kijana mzuri sana Jerry Silaa, nilianza nae kwenye Sekta ya ardhi, mmeona kazi kubwa aliyoifanya kwenye ardhi, kazi ya kuendesha kliniki za kutosha kutatua kero za ardhi Tanzania, sasa kwa kazi kubwa aliyoifanya nimeona sasa nimkabidhi vyombo vya habari na propaganda zetu zote za Tanzania”
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania