#HABARI: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan, amepongeza mpango wa utunzaji mazingira unafaonywa na Kiwanda cha Mkwawa, katika ukaushaji wa zao la Tumbaku kwa kutumia Jua badala ya kutumia kuni na kuwataka wawekezaji kutumia teknolojia hiyo kusambaza kwa wakulima ili kuepuka dhana ya uharibifu wa mazingira unafaonywa na wakulima wa zao hilo.
Rais Samia amesema hayo wakati akiweka jiwe la msingi ujenzi wa Kiwanda cha kutengeneza Sigara cha Serengeti Cigarette Company Ltd, kilicho chini ya kampuni ya Mkwawa Leaf na kubainisha kiwanda hicho kitaongeza fursa kubwa ya ajira kwa wananchi wa Mkoa wa Morogoro.