#HABARI: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe

#HABARI: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema mfumo wa gridi ya Taifa una umeme wa kutosheleza mahitaji ya kijamii na kiuchumi.

Rais Samia ameyasema hayo wilayani Gairo, Mkoa wa Morogoro akiwa katika ziara ya kikazi.

Rais Samia amesema, serikali inazidi kuimarisha hali ya upatikanaji umeme nchini kupitia ujenzi na ukarabati wa miundombinu, ambapo imejenga kituo cha kupokea na kupoza umeme wilayani Kongwa, mkoani Dodoma, ambacho kitaboresha pia hali ya umeme wilayani Gairo.