#HABARI: Nyumba zaidi ya 1500 katika mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara na Lindi, zimeunganishwa kwenye Nishati safi ya kupikia, lengo ifikapo mwaka 2034, asilimia themanini ya watanzania waweze kutumia nishati hiyo.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Newala Alhaji Rajabu Kundya, ambapo amelitaka shirika la TPDC, kuongeza nguvu ili kufikia idadi kuwa ya Watanzania ambao anaathirika na nishati chafu ya kupikia.
Amesema idadi kubwa ya Watanzania bado wanatumia kuni na mkaa kupikia na hivyo kuathirika kiafya hasa maeneo ya Vijijini, ambapo matumizi ya nishati chafu ni makubwa zaidi.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania