#HABARI: Naibu Waziri wa Uchukuzi Mh

#HABARI: Naibu Waziri wa Uchukuzi Mh. David Kihenzile, amezitaka Sekta binafsi za ndani na nje ya nchi kujitokeza kuwekeza kwa kununua Ndege za kutoa huduma kwa abiria na mizigo badala ya kuitegemea serikali,ambayo imevifanyia maboresho viwanja vyote vya ndege nchini ili kusaidia baadhi ya Mikoa yenye uhitaji.

Naibu Waziri Kihenzile,ameyazungumza hayo baada ya kukagua na kupokea taarifa ya uboreshaji, katika kiwanja cha ndege cha Tanga.