#HABARi: Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe.David Silinde, ameielekeza Kampuni ya Mbolea ya Taifa (TFC) kuhakikisha wakulima wote nchini wanapata mbolea ya ruzuku kwa wakati, ili kuwasaidia kuongeza uzalishaji wa mazao ili kufikia azma ya Serikali kuhakikisha Sekta ya Kilimo inakuwa kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030.
Naibu Waziri ametoa maelekezo hayo katika Maonesho ya Kilimo Nanenane, katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma, alipofika kwenye banda la TFC.
Naye Afisa Masoko wa TFC Bw. Laurent Otaru, miongoni mwa mikakati waliyonayo ni kuongeza idadi ya mawakala wapya watakosaidia kusambaza mbolea kwa urahisi, na kushirikiana na Vyama vya Ushirika ili kuwafikia wakulima wengi zaidi hususani maeneo ya Vijijini.