#HABARI: Mtoto Malick Hashimu (6) mkazi wa Goba Dar es Salaam, ambaye alijeruhiwa na kitu chenye ncha kali shingoni na mfanyakaz…

#HABARI: Mtoto Malick Hashimu (6) mkazi wa Goba Dar es Salaam, ambaye alijeruhiwa na kitu chenye ncha kali shingoni na mfanyakazi wa ndani, ameruhusiwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya hali yake kuimarika.

Julai 17, 2024 Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, lilitoa taarifa ya kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo, Clemensia Cosmas Mirembe (19) akiwa amejificha kwenye ‘Pagala’ maeneo ya Goba Kizudi Kinondoni.

Taarifa ya Polisi ilieleza kuwa mtuhumiwa huyo anahojiwa kwa kina na atafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo kwa hatua zaidi za Kisheria.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow @radioonetanzania