#HABARI: Msemaji wa Jeshi la Polisi, Naibu kamishna wa Polisi DCP – David Misime, amesema Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne Jijini Dar es Salaam, waliokiuka sheria na kusambaza picha mjongeo wa tukio la udhalilishaji wa kijinsia, kwenye mitandao ya kijamii, ambao ni Frora Mlombola, Aghatha Mchome, Madatha Jeremiah Budodi na James Nyanda Paulo.