#HABARI: Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof.Mohamed Janabi, amesema ugonjwa wa tezi dume ndiyo ugonjwa pekee, unaoongoza kwa wanaume kuliko saratani nyingine yeyote, huku akiwataka vijana kujenga utamaduni wa kupima na kuacha fikra kwamba ugonjwa huo huwapata wazee pekee.
Prof.Janabi ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza kupima magonjwa ya saratani ya shingo ya uzazi kwa wanawake, tezi dume pamoja na kisukari katika kituo cha afya cha Mtakanini kilichopo Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.
Amewatoa hofu wananchi kuhusu taratibu za upimaji wa ugonjwa huo na kwamba kwa sasa wanatumia kipimo rahisi cha damu hivyo wajitokeza kwa wingi.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania