#HABARI: Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw

#HABARI: Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Abdul-Razaq Badru, amewaongoza watumishi wa mfuko huo kutoa huduma na elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa Wanachama na Wananchi wanaotembelea banda la Mfuko kwenye viwanja vya Nzuguni Dodoma ambako maonesho hayo yanafanyika kitaifa.

Huduma kama hizo zimekuwa zikitolewa na Maafisa wa PSSSF kwenye Maonesho ya Nanenane yanayoendelea kwenye Kanda za Nyanda za Juu Kusini katika viwanja vya John Mwakangale, Jijini Mbeya na kwenye viwanja vya Dole Kisiwani Unguja, Zanzibar.