#HABARI: Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umeendelea kutoa huduma kwa wananchama na wanachama kwa ujumla …

#HABARI: Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umeendelea kutoa huduma kwa wananchama na wanachama kwa ujumla wakati huu wa Maonesho ya Nanenane 2024 yanayofanyika kitaifa katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

Pia PSSSF wanatoa huduma kwenye Maonesho ya Nanenane yanayoendelea kwenye Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Zanzibar kwenye viwanja vya Dole, Unguja.

Kwa mujibu wa Afisa Uhusiano, PSSSF, Bi. Rehema Mkamba amesema Maonesho hayo ni fursa nzuri kwa mfuko kukutana na wanachama wake, wakiwemo wananchi ili kutoa huduma ikiwa ni pamoja na elimu ya hifadhi ya Jamii.

Alisema Mwanachama akifika kwenye mabanda ya PSSSF, ataweza kupata taarifa za Michango, Taarifa za Mafao, Taarifa za Uwekezaji unaofanywa na Mfuko na Wastaafu wataweza kujihakiki.