#HABARI: Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imefanikiwa kuokoa upotevu wa fedha za serikali kiasi cha TZS: 567,636,151,9…

#HABARI: Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imefanikiwa kuokoa upotevu wa fedha za serikali kiasi cha TZS: 567,636,151,996.00 katika mshauri 140 yaliyokuwa katika hatua mbalimbali za michakato ya ununuzi wa umma kwa kipindi cha miaka mitatu (2021 – 2024).

Katibu Mtendaji wa PPAA, Bw. James Sando amebainisha hayo katika viwanja vya Nzuguni, Jijini Dodoma.

“PPAA imeendelea kudhibiti taasisi nunuzi kukiuka taratibu za kisheria hasa katika kufanya tathmini ya zabuni (tender evaluation); katika baadhi ya mashauri ambapo ilifanikiwa kubaini ukiukwaji wa taratibu za kufanya tathimini uliofanywa na taasisi nunuzi ikiwemo kutokuzingatia vigezo vilivyowekwa katika kabrasha la zabuni au kuongeza vigezo vipya ambavyo havikuwepo awali.” amesema Bw. Sando.