#HABARI: Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mhe

#HABARI: Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali itaendelea kujenga shule kubwa na za kisasa zitakazokidhi mahitaji yote ya wanafunzi kuanzia ngazi ya Msingi hadi Sekondari ili kuwaondolea changamoto Wanafunzi ya kuingia mikondo miwili jambo ambalo linarejesha nyuma maendeleo ya elimu nchini.

Akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Shule ya Msingi Kojani, Makamu wa Pili wa Rais amesema dhamira ya Rais Dkt.Mwinyi ni kuhakikisha kila mtoto wa kizanzibari anapata haki yake ya msingi ya kusoma katika mazingira mazuri yatakayozalisha wataalamu wa fani mbalimbali watakaolisaidia taifa katika harakati za maendeleo.