#HABARI: Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman, ametaka jamii nchini, kuhakikisha kwamba inatunza na kut…

#HABARI: Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman, ametaka jamii nchini, kuhakikisha kwamba inatunza na kuthamini ipasavyo rasilimali ya bahari iliyopo Zanzibar pamoja na mazingira nchini, ili viweze kuwa na tija na manufaa zaidi kwa taifa.

Mhe.Othman ametoa kauli hiyo huko Makangale Wilaya ya Micheweni, alipozungunza katika ziara ya kutembelea utunzaji mazingira kwenye hoteli ya Manta Resort, kiwanda cha kuongeza thamani samaki, soko la samaki pamoja na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa madarasa ya Skuli ya Mnarani inayojengwa kwa malighafi ya chupa za plasiti.

Mhe.Othman amewaeleza wananchi kwamba bahari iliyopo na mazingira ndio rasilimali muhimu kwa wananchi wengi wa
Zanzibar, na kwamba wanawajibu wa kuhakikisha kwamba inatunzwa kwa manufaa ya wazanzibari wote.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow @radioonetanzania