#HABARI : Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA bara Mhe.Tundu Lissu, amesema zoezi la kupiga kura kwenye uchaguzi wa kuwapata Viongozi w…

#HABARI : Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA bara Mhe.Tundu Lissu, amesema zoezi la kupiga kura kwenye uchaguzi wa kuwapata Viongozi wapya wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (Tanganyika Law Society – TLS) limeenda vizuri kama lilivyopangwa.

Lissu ametoa kauli hiyo leo, wakati wa zoezi la kupiga kura kwenye uchaguzi wa kuwapata viongozi linaloendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma, unapofanyika mkutano Mkuu wa chama hicho.