#HABARI: Katika kuhakikisha ulinzi na Elimu vinatolewa, Jeshi la Polisi kupitia kikosi cha Wanamaji nchini kimeyafikia makundi mbalimbali yawatumiaji wa vyombo vya majini ambapo, kimetoa elimu ya ukatili wa kijinsia na mbinu za namna bora za kujiokoa pindi inapotokea ajali katika vyombo hivyo.
Akitoa elimu hiyo, katika Boti ya Kilimanjaro Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto kutoka kikosi cha wanamaji Mkaguzi wa Polisi INSP Avelina Temba, amewaomba wananchi hao kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyofanywa na baadhi ya watu wasio na maadili katika jamii.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania