#HABARI: Katika kuhakikisha hali ya usawa inapatikana katika elimu, Benki ya CRDB, imetoa jumla ya magodoro 160 kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum wanaotarajia kuanza kukaa bweni katika shule ya msingi Katete, iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma, wilayani Momba, mkoani Songwe.
Msaada huo wa magodoro umepokelewa na Mkuu wa Mkoa huo Bw. Daniel Chongolo, ambaye licha ya kushukuru na kuipongeza benki hiyo amesema jamii inapaswa kuwakumbuka na kuwalinda watoto wenye uhitaji maalum kwani miongoni mwao wapo wenye vipaji na kupitia elimu wanaweza kutimiza ndoto zao na kuwa msaada kwa taifa.
Akielezea msaada huo Meneja wa CRDB, Tawi la Tunduma, Bw. Crispin Kombo, amesema magodoro ,meza na viti walizotoa zenye thamani ya shilingi milioni 10 ni sehemu ya kurejesha kwa jamii huku akiwataka wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwaficha watoto wenye mahitaji maalum.