#HABARI: Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof

#HABARI: Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe, amesema ameridhishwa na maandalizi ya Maonesho ya Nanenane yaliyofanywa na Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kwa lengo la kutoa elimu kwa wafugaji na wadau mbalimbali kuhusiana na huduma zinazotolewa na TVLA kwenye maonesho hayo ambayo kitaifa yanafanyika katika Uwanja wa Nzuguni Jijini Dodoma hadi 8 Agosti, 2024

Prof. Shemdoe amekagua huduma hizo leo, alipotembelea taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa lengo la kujiridhisha na huduma zitakazotolewa kwa Wafugaji, Wavuvi na wadau mbalimbali watakaotembelea Maonesho hayo.

Huduma zilizokaguliwa na Katibu Mkuu kwenye banda la TVLA ni pamoja na elimu ya uchunguzi wa Magonjwa ya Wanyama, elimu ya matumizi sahihi ya Chanjo za Mifugo, elimu ya uhakiki wa ubora wa vyakula vya Mifugo, elimu ya usajili na uhakiki wa ubora wa viuatilifu vya Mifugo, elimu ya utafiti wa magonjwa ya wanyama pamoja na elimu kuhusiana na mafunzo kwa wataalamu wa Mifugo inayotolewa na TVLA.