#HABARI: Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Eliakim Maswi, amewataka watumishi wa Wizara hiyo kuwajibika katika majukumu yao, ili kutimiza malengo ya Wizara na matarajio ya wananchi.
Maswi ameyasema hayo wakati wa makabidhiano ya Ofisi kati yake na Bi. Mary Makondo aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala mkoa wa Ruvuma, katika Ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma.
“Nawaomba mambo makubwa mawili; kwanza, nahitaji utumishi uliotukuka, utumishi huo uambatane na ushirikiano bila majungu wala makundi. Pili, nahitaji watumishi wawajibikaji.” Alisema na kuongeza “Tumeomba kazi wenyewe na wengine tumetoka vijijini kwetu sasa tufanye kazi”