#HABARI: Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, ameitaka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kuongeza kasi ya kufanya tafiti za aina nyingine za Chanjo za Mifugo ambazo hazijaanza kuzalishwa ili kukidhi mahitaji ya wafugaji nchini.
Dkt. Kusiluka ameyasema hayo alipotemblea banda la TVLA akiambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe, lililopo kwenye banda jumuishi la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Nanenane) yanayoendelea kufanyika katika uwanja wa Nzuguni jijini Dodoma.