#HABARI: Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dk.Moses Kusiluka ametoa wito kwa vijana kujihusisha na usindikaji wa kisasa wa bidhaa za kilimo kwani kilimo kina fursa na pia kilimo ni biashara kubwa na teknolojia zinazotumika ni za kisasa.
Balozi Dk. Kusiluka amayasema hayo alipotembelea katika Maonesho ya Kimataifa ya Nanenane katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma akiambatana na Katbu Mkuu Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe.