#HABARI: Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Legal Aid, ambayo imekuwa ikihudumia wananchi wanaohitaji msaada wa Kisheri…

#HABARI: Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Legal Aid, ambayo imekuwa ikihudumia wananchi wanaohitaji msaada wa Kisheria, imeendelea kugusa makundi ya wananchi wa hali ya chini, ambapo wananchi waliofikiwa na Msaada huo wa Kisheria Jijini Dodoma, wengine wakitoka mikoa mbalimbali nchini, wamesaidiwa katika eneo la Mirathi na wakimuomba Rais wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, msaada huo ufike zaidi kwa wananchi waishio Vijijini kwani wamekuwa wakikumbana na changamoto zinazohitaji msaada wa Kisheria.

Wananchi waliofika kwenye banda la Wizara ya Katiba na Sheria, kwenye viwanja vya maonesho ya Nanenane Nzuguni Jijini Dodoma, wamesema wameridhishwa na msaada waliopatiwa.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow @radioonetanzania