#HABARI: Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum la Dar es Salaam, Muliro Jumanne Muliro, amesema binti anayedaiwa kulawitiwa na…

#HABARI: Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum la Dar es Salaam, Muliro Jumanne Muliro, amesema binti anayedaiwa kulawitiwa na kubakwa bado yupo hai hajafa, kama ambavyo taarifa zimekuwa zikisambaa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii.

Kamanda Muliro, amesema Jeshi hilo linamshikilia Mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Amos Lwiza (54) mkazi wa Tegeta wilaya ya Kinondoni anayedaiwa kusambaza taarifa hiyo mitandaoni.

Aidha Kamanda Muliro amesema wanaendelea na uchunguzi kwa waliohusika kwenye tukio la ubakaji na ulawiti.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow @radioonetanzania