#HABARI: Jeshi la Polisi mkoani Geita, linamshikilia Flora Mapolo (33) mkazi wa Kitongoji cha Mlima namba tano, Kata ya Lwamgasa mkoani Geita, akidaiwa kumnyonga mmoja wa watoto wake wawili waliozaliwa mapacha, wakiwa na miezi miwili kisha kumtupa porini huku mwili wa mtoto huyo ukikutwa umenyofolewa mguu na mkono hali iliyozua taharuki kwa jamii.
Kamanda wa Polisi mkoani Geita Kamishina Msaidizi, Mwandamizi wa Polisi, Safia Jongo, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema Jeshi hilo linaendelea na uchunguzi kubaini watu waliohusika kumnyofoa viuongo mtoto huyo mchanga mwenye umri wa miezi miwili.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania