#HABARI: Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, linawashikilia watuhumiwa wawili kwa tuhuma za kusambaza taarifa za uongo katika mitand…

#HABARI: Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, linawashikilia watuhumiwa wawili kwa tuhuma za kusambaza taarifa za uongo katika mitandao ya kijamii, kuhusiana na video ya binti mmoja aliyefanyiwa ukatili hivi karibuni huko Jijini Dar es Salaam, wakidai kuwa amefariki dunia suala ambalo sio kweli.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo, amethibitisha na huku akibainisha kuwa Jeshi hilo linaendelea na upelelezi wa shauri hilo na pindi utakapokamalika jalada litapelekwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria.

Ametoa wito kwa wananchi kuepuka kusambaza ama kuchapisha taarifa za uongo kwenye mitandano ya kijamii kwa lengo la kuleta taharuki au kutafuta umaarufu kuacha mara moja kwani ni makosa na wataendelea kuchukua hatua za kisheria dhidi yao.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow @radioonetanzania