Gwiji wa uzani wa Heavyweight George Foreman afariki akiwa na umri wa miaka 76

Gwiji wa uzito wa juu kutoka Marekani George Foreman amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 76, familia yake imetangaza Ijumaa.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Foreman, bingwa wa zamani wa dunia, aliingia katika historia ya ndondi baada ya kushindwa na Mohamed Ali katika pambano maarufu la “Rumble in the Jungle” mnamo 1974 huko Kinshasa.

“Ni kwa huzuni kubwa kwamba tunatangaza kufariki kwa mpendwa wetu George Edward Foreman Sr., ambaye ameaga dunia kwa amani mnamo Machi 21, 2025, akiwa amezungukwa na wapendwa wake,” familia yake imeandika katika taarifa.

“Mwanabinadamu, Mwana Olimpiki, bingwa wa dunia mara mbili, aliheshimiwa sana. Alikuwa mtu mwenye nguvu, mtu wa nidhamu, mwenye kusadiki, mlinzi wa urithi wake, ambaye alipigana bila kuchoka ili kuhifadhi jina lake, kwa ajili ya familia yake. “

George Foreman, mwenye uwezo unaopita ubinadamu, alikua bingwa wa dunia kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1973 kwa kumshinda Joe Frazier, baada ya kuwa bingwa wa Olimpiki mnamo mwaka 1968 huko Mexico.

Bondia huyo mwenye asili ya kitongoji cha watu weusi cha Houston, alipigwa na Mohamed Ali mwaka 1974 mjini Kinshasa mbele ya karibu watazamaji 100,000, akizidiwa na uvumilivu, mbinu na ujanja wa kabla ya kupambana na mpinzani wake, ambaye alishinda umati mzima.

Pambano hilo linasalia kuwa moja ya pambano kubwa zaidi katika historia ya ndondi, kutokana na kiwango na ukali wake.

Foreman alitundika glavu zake akiwa na umri wa miaka 28, akiingia kwenye dini, kabla ya kurejea ulingoni miaka kumi baadaye huku kurudi kwake kuliwashangaza wengi.

Baada ya kushindwa mara mbili kwa taji jipya, akawa bingwa wa dunia tena mwaka wa 1994 akiwa na umri wa miaka 45 dhidi ya Michael Moorer, kabla ya kustaafu mwaka wa 1997 akiwa na umri wa miaka 48.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *