Guterres amuonya Trump kuhusu jaribio la kufuta kizazi cha Wapalestina huko Gaza

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ameonya dhidi ya jaribio lolote la “kufuta kizazi” cha Wapalestina huko Gaza, akisisitiza haja ya kuzingatiwa sheria za kimataifa wakati wa kutafuta ufumbuzi wa suala la Palestina.