Guterres aitaka Israel kusitisha ukiukaji wa azimio nambari 1701 kusini mwa Lebanon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ameitaka Israel ikomeshe kukalia kwa mabavu ardhi ya Lebanon na kufanya operesheni za kijeshi ndani ya nchi hiyo, akisisitiza kuwa vitendo hivi vinakiuka azimio nambari 1701 la Baraza la Usalama.