Guinea: Waziri Mkuu atangaza ‘kurejea kwa utaratibu wa kikatiba’ mnamo 2025

Kiongozi wa serikali ya Guinea Amadou Oury Bah ametangaza kwa vyombo vya habari siku ya Jumatano kura ya maoni na uchaguzi wa urais na wabunge mwaka 2025, mwaka ambao “kurejeshwa kwa utaratibu wa kikatiba kutakuwa na ufanisi” nchini humo, baada ya serikali ya kijeshi iliyotawala tangu mwaka 2021 kushindwa kutimiza ahadi yake ya kurejesha mamlaka kwa raia mwaka 2024.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Conakry, Mouctar Bah

Katika kutangaza kurejea kwa utaratibu wa kikatiba, mkuu wa serikali hakutetereka: “Tunachopaswa kukumbuka mwaka wa 2025, kurejea kwa utaratibu wa kikatiba kutakuwa na ufanisi katika kura ya maoni, uchaguzi wa urais, uchaguzi wa wabunge. “Anataja kuwa bado kuna msururu wa ugumu ambao utalazimika kuondolewa. “Muda unajadiliwa, kwa sababu ugumu mkubwa ambao tutalazimika kuondoa ni katiba ya daftari la uchaguzi. Daftari la uchaguzi linaweza kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani katika baadhi ya nchi.

Katika kujibu maswali mengi kutoka kwa waandishi wa habari, masuala kuhusi visa vya utekaji nyara na kutoweka kwa wakosoaji au wapinzani ambao walishtakiwa kimakosa, pia yamejadiliwa. “Ninaweza kusema kwamba kila kitu ambacho kimetokea tangu mwezi wa Julai 2024 na kutoweka kwa Foniké Mengué na Billo ni jambo ambalo halijaambatana na maslahi ya serikali. Tuna uzoefu wa kila kitu kilichotokea katika miaka ya hivi karibuni kulaumu mamlaka kwa hali ambazo zinachochewa mahali pengine.”

Mkuu wa nchi katika hotuba yake kwa taifa mwishoni mwa mwaka 2024 alisema kuwa mwaka 2025 ungekuwa mwaka muhimu wa uchaguzi bila kutoa ratiba.