
Ujumbe wa ECOWAS ulitembelea Guinea-Bissau kati ya Februari 21 na 28 kusaidia kutatua mzozo wa kisiasa kuhusu kupanga tarehe ya uchaguzi wa urais. Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa siku ya Jumapili, Machi 2, ujumbe huo umesema uliondoka nchini “mapema Jumamosi asubuhi kufuatia vitisho vya kufukuzwa vilivyotolewa na Rais Umaro Sissoco Embalo.”
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Katika timu ya upatanishi ya ECOWAS, Balozi Babatunde O. Ajisomo, mshauri wa mkuu wa ujumbe huo, na Serigne Mamadou Ka, mtaalamu kutoka tume ya uchaguzi, walipewa jukumu la kutafuta suluhu za kudumu za kuleta amani nchini Guinea-Bissau, kwa kuzingatia mwafaka wa kisiasa kabla ya uchaguzi uliopangwa kufanyika Novemba 30.
Mfumo unaoudhi
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, ujumbe wa ECOWAS umeeleza kwamba “ulipokelewa kwa hadhira na Rais Umaro Sissoco Embalo” na kisha “kufanya mashauriano na wadau mbalimbali katika ngazi ya taifa” ili kufikia “makubaliano” ya kufanyika kwa uchaguzi mwaka 2025 nchini Guinea-Bissau.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa siku ya Jumapili, Machi 2, ujumbe huo umesema uliondoka nchini “mapema Jumamosi asubuhi kufuatia vitisho vya kufukuzwa vilivyotolewa na Rais Umaro Sissoco Embalo.” Ujumbe huo ulikutana na viongozi wa upinzani. Mbinu ambayo ilimkasirisha mkuu wa nchi, ikiwa tutamwamini Aristides Gomes, waziri mkuu wa zamani wa nchi: “Sissoco alikuwa nje ya nchi, lakini alikuwa na habari. Mara tu uumbe huo ulipokubali matakwa ya upinzani na kukutana na viongozi wake, misheni hiyo ilikiuka lengo kuu la Sissoco, ubinafsishaji wa madaraka. “
Si mara ya kwanza mvutano kama huo kutokea
Hii si mara ya kwanza kwa Umaro Sissoco Embalo kuzozana na ujumbe wa ECOWAS nchini mwake. “Sissoco anaendana na yeye mwenyewe. Alipojitangaza kuwa rais kwa kuungwa mkono na vikosi vya usalama, aliwafukuza wajumbe wa ECOWAS waliokuwa Guinea-Bissau na kutangaza wawakilishi wao wa ECOWAS nchini humo kuwa watu wasiostahili,” anakumbusha Aristides Gomes.
Licha ya hali hiyo, tatmini ya ujumbe huo itatumwa hivi karibuni kwa rais wa tume ya ECOWAS.