Guinea-Bissau: Rais Embalo asogeza mbele uchaguzi wa rais na wabunge kwa wiki moja

Uchaguzi wa rais na wabunge nchini Guinea-Bissau utafanyika tarehe 23 Novemba. Wiki moja mapema kuliko tarehe ya Novemba 30 iliyotangazwa hapo awali. Hii inabainishwa na agizo kutoka kwa rais. Umaro Sissoco Embalo aliitisha mkutano na vyama siku ya Ijumaa Machi 7, 2025, wakati nchi hii inapitia mzozo wa kisiasa. Mkutano huo ulisusiwa na muungano mkuu wa upinzani, unaozingatia kuwa muhula wa mkuu wa nchi ilimalizika tarehe 27 Februari.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Itakuwa Novemba 23, badala ya tarehe 30 Novemba. Tarehe ya uchaguzi wa urais na wa wabunge nchini Guinea-Bissau imesogezwa mbele kwa wiki moja, kwa mujibu wa agizo la rais iliyochapishwa Ijumaa Machi 7. Sheria inasema uchaguzi unapaswa kufanyika kati ya Oktoba 23 na Novemba 25, amehalalisha Umaro Sissoco Embalo. Tangazo hilo lilitolewa kufuatia mashauriano na vyama vya siasa, kwa mwaliko wa rais wa Guinea-Bissau, ili kupata mwafaka wa tarehe ya uchaguzi mkuu, wakati nchi inapitia mgogoro wa kisiasa.

Mkutano bila muungano mkuu wa upinzani

Lakini mkutano huo ulifanyika bila muungano mkuu wa upinzani, Pai Terra Ranka, unaongozwa na Domingos Simoes Perreira. Mpinzani na Waziri Mkuu wa zamani alitoa wito wa kususia uchaguzi huo, akiona mbinu hiyo kama njia ya mkuu wa nchi “kuelekeza umakini ili kupata wakati wa kutosha mamlakani.” Upinzani unaona kuwa muhula wa rais umekwisha, tangu alipoapishwa Februari 27, 2020 kwa muhula wa miaka 5, ingawa uamuzi wa Mahakama ya Juu ulirudisha nyuma tarehe ya mwisho hadi Septemba 4.

Mapema wiki hii, Umaro Sissoco Embalo alijitangaza kuwa mgombea kwenye kiti chake cha rais.