Guinea-Bissau: Rais anayemaliza muda wake Embalo atangaza kugombea kiti cha urais

Rais Umaro Sissoco Embalo amerejea Guinea-Bissau siku ya Jumatatu, Machi 3, baada ya ziara yake huko Ulaya. Ametangaza kugombea kiti cha urais, huku akihakikisha kuondoka kwa haraka kwa ujumbe wa ECOWAS, ambao ulikuja nchini kujaribu kupunguza mvutano katika ya wanasiasa.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Umaro Sissoco Embalo ni mgombea kwa kiti cha urais anachoshikilia kwa sasa. Rais wa Guinea-Bissau ametangaza siku ya Jumatatu kwamba atawania muhula wa pili katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Novemba 30.

Rais atangaza kugombea

Kurudi Bissau baada ya mfululizo wa ziara rasmi, ikiwa ni pamoja na Moscow na Paris, Rais Embalo aliondoka kwenye ndege wakati tayari alionyesha kugombea kwake na ushindi wake katika duru ya kwanza.

Rais pia amekiri kutoa agizo la kufukuza ujumbe wa ECOWAS, uliokuwa umetumwa huko Bissau wiki iliyopita: “Hawakuheshimu kile kinachotakiwa kufanyika. Hii si jamhuri ya kima mtu kuleta hoja zake. Kuna rais, kuna sheria, kuna Katiba. Na Mahakama ya Juu, hatufanyi mzaha kuhusu hilo. “

Misheni hii, ni mimi niliyetoa amri ya kufukuzwa, ni mimi niliyewafukuza hapa.

Tangu lilipovunjwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita, Desemba 2023, hakujakuwa na Bunge. Upinzani sasa unamchukulia Rais Embalo kuwa sio rais halali, ukibaini kwamba muda wake wa sasa uliisha mwishoni mwa mwezi Februari.

Baada ya kuja kwa ujumbe wa uchunguzi juu ya sula hili, ujumbe wa ECOWAS, kulingana na vyanzo vilivyo karibu na Umaro Sissoco Embalo, ulivuka mamlaka yake kwa kufanya mazungumzo na upinzani, hasa miungano ya PAI-Terra Rank na API Cabas Garandi.

Kwa tishio la kufukuzwa, wajumbe walipendelea kuondoka Bissau alfajiri ya Jumamosi Machi 1. Tamko la mwisho kutoka ECOWAS linatarajiwa, hasa kinachotakiwa kufanyika kwa uchaguzi wa wabunge na urais.