Greenwood anaweza kutua huku

Hivi karibuni staa wa Marseille, Mason Greenwood, amekuwa hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza na kocha wa timu hiyo Robert de Zerbi ameweka wazi kwamba haridhishwi na utendaji kazi wake, hivyo anatakiwa abadilike kama anataka kupata nafasi.

Taarifa nyingine zimeripoti kwamba kwa sababu hiyo, kuna uwezekano mkubwa Marseille ikaachana na mshambuliaji huyu mwisho wa msimu endapo atashindwa kufanya kile ambacho kocha anahitaji, jambo ambalo linapewa asilimia nyingi. Lakini je, akiuzwa anaweza kutua wapi? Hizi hapa timu tano zinazoweza kumsajili fundi huyu.

Alipokuwa akiichezea Getafe kwa mkopo, mara kadhaa Barcelona walituma wawakilishi wao kwa ajili ya kwenda kumtazama katika mechi za La Liga ambazo alikuwa akicheza.

Kutokana na hali yao ya kiuchumi, miamba hii ya Nou Camp ilipanga kumchukua kwa mkopo utakaokuwa na kipengele cha kumnunua jumla staa huyu ambaye anaendana na falasafa zao kutokana na umri wake na waliona angeingia kirahisi katika kikosi chao kilichojaa vijana.

Baada ya kufeli kwa wakati huo kwa sababu Man United ilihitaji kumuuza na sio kumtoa kwa mkopo, Barcelona bado ina mpango na fundi huyu ambaye kwa mujibu wa watu wake wa karibu, alipenda sana kuendelea kukaa Hispania.

Saudi Arabia ni kati ya sehemu ambazo wachezaji wengi wamekuwa wakikimbilia kutokana na  mkwanja wa kutosha ambao timu za huko zinatoa.

Greenwood pia anaonekana kuwa huenda akatua huko hususani Al Nassr ambayo ina Cristiano Ronaldo ambaye Greenwood anamkubali sana.

Mara kadhaa Al Nassr imehusishwa na Greenwood lakini mchakato ulifeli.

Staa huyu anaonekana kuwa na uhitaji wa kuendelea kubaki barani Ulaya na kucheza Ligi ya Mabingwa kitu ambacho timu hiyo haiwezi kumpa, ingawa katika upande wa pesa wana mzigo wa maana.

Kabla ya kwenda Marseille, hii ilikuwa ni mojawapo ya timu zilizokuwa katika vita ya kuiwania saini yake lakini ikashindwa.

Juventus ilikuwa tayari kufanya hadi mabadilishano ya wachezaji na Man United kwa wakati huo ili kuhakikisha staa huyu anatua katika mikono yao lakini mambo yalikwenda tofauti na akatua zake Marseille.

Kutokana na uwezekano wa kuuzwa mwisho wa msimu huu, Juventus bado inadaiwa kuwa na uhitaji wa huduma yake na inaweza kumsajili.

ATLETICO MADRID

Ni timu nyingine kutoka La Liga mbali ya Barcelona ambayo ilihusishwa kutaka kumsajili Greenwood tangu mwaka jana kabla hajatua Marseille.

Atletico ilishindwa kumpata fundi huyu kutokana na ada kubwa ya uhamisho ambayo ilitajiwa na Man United kwa wakati huo.

Kutokana na uwezekano wa kumpata kwa sasa, kuna uwezekano vijana hao wa Diego Simeone wakakaa mezani na Marseille.

Lazio ilikuwa katika hatua nzuri kumsajili Greenwood kabla hajajiunga na Getafe katika dirisha la majira ya baridi mwaka jana.

Taarifa zinadai Greenwood mwenyewe alishakubali na kila kitu kilikuwa sawa lakini dili likafeli siku ya mwisho ya usajili kutokana na kutotimia kwa baadhi ya dokumenti.

Katika mahojiano yake akielezea dili hilo rais wa Lazio, Claudio Lotito, alisema: “Nilijaribu hadi dakika ya mwisho.”

Inaelezwa timu hiyo bado inahitaji saini yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *