
Waziri Mkuu mpya wa Greenland amesema Jumapili, Aprili 27, kwamba kisiwa kikubwa cha Arctic hakitakuwa “mali” ya kuuzwa, akitaja maoni ya Marekani kuhusu kunyakua eneo linalojitawala la Denmark ni kukosa heshima.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Wakati wa ziara yake nchini Denmark Jumapili, Aprili 27, Waziri Mkuu mpya wa Greenland, Jens-Frederik Nielsen, amefutilia mbali suala la kunyakuliwa kwa Marekani.
“Hatutawahi kuwa mali ambayo mtu yeyote anaweza kununua, na huo ndio ujumbe ambao nadhani ni muhimu zaidi kuuelewa,” Jens-Frederik Nielsen amewaambia waandishi wa habari pamoja na Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen wakati wa ziara yake ya kwanza nchini Denmark tangu aingie madarakani.
Donald Trump anaendelea kusema: anaitamani Greenland. Lakini eneo linalojiendesha la Denmark linaweka upinzani. Wakati wa ziara yake ya kwanza nchini Denmark tangu chama chake cha mrengo wa kulia, The Democrats, kushinda uchaguzi wa bunge mwezi Machi, Waziri Mkuu mpya wa Greenland, Jens-Frederik Nielsen, amekariri kwamba kisiwa kikubwa cha Arctic hakitakuwa “mali” ya kuuzwa.
“Hatutawahi kuwa mali ambayo mtu yeyote anaweza kununua, na huo ndio ujumbe ambao nadhani ni muhimu zaidi kuuelewa,” amesema.
“Sasa tunajikuta katika hali ambayo lazima tubaki na umoja,” mkuu wa serikali ya Greenland ameongeza, kabla ya kusema kwamba “maoni yaliyotolewa na Marekani (juu ya kunyakua Greenland) hayakuwa ya heshima.” “Ninakubali kabisa,” ameongeza Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen.
“Huwezi kunyakua nchi nyingine,” Waziri Mkuu wa Denmark alitangaza nchini Marekani wakati wa ziara yake katika eneo la Arctic mapema mwezi Aprili.