Waathiriwa wa mapigano kati ya M23 na FARDC ambao kwa sasa wanaiishi kwenye kambi za wakimbizi huko Goma mashariki mwa DRC,wamelalamikia kulazimishwa kuondoka kambini wakati huu hali ya wasiwasi ikiendelea kushuhudiwa katika mkoa wa Kivu kaskazini na kusini.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Wasiwasi inaedelea kushuhudiwa licha ya wakuu wa EAC na SADC kutoa wito kwa pande hasimu kusitisha mapigano.
Mama Chantal Sanju na Boniface Kaluke ni raia waliokimbia mapigano kati ya M23 na FARDC wilayani Masisi na ambao wamekuwa wakiishi katika kambi ya Kanyaruchinya, miaka mitatu baadae walilazimishwa kuondoka kwenye kambi hiyo. Kwa sasa wapo kwenye kambi ya Bulengo ambapo wanasema pia wanalazimishwa kuondoka wakielekeza kuwa hatarani.
“Sisi sote wakimbizi hatuna makao tunaomba kutafutiwa makao na mahali pa kukaa, kuliko kutufukuza, Nina uja uzito pamoja na walemavu, Kahembe watuhamishe na Muja watubomolee tunaanza kwenda ambapo hatufahamu.”Walisema wakimbizi mjini Goma.

Watetezi wa haki za binaadamu na Mashirika ya kiraia wametoa wito kwa pande hasimu kuheshimu haki za binadamu wakati wa vita. Pacifique Kararuka ni mtetezi wa haki za binadamu mjini Goma.
“Tunataka hizi serikali mbili ambazo zinazozana watazame vile watalinda raia, wawe FARDC au M23 walinde raia ili raia wapate usalama wakudumu.”AlielezaPacifique Kararuka ni mtetezi wa haki za binadamu mjini Goma.
Katika hatua nyengine, Ofisi ya kuratibu misaada ya binadamu katika Umoja wa Mataifa OCHA, imetangaza kuwa watu zaidi ya watu 32 000 waliohamishwa walirudi katika vijiji vyao maeneo ya Kasizi Buhumba na Kigatame wilayani Nyiragongo. OCHA imesisitizia hitaji la upatikanaji wa maji,ukarabati wa malazi, ujenzi wa makazi yaliyoharibiwa, ulinzi na elimu.
CHUBE NGOROMBI GOMA RFI KISWAHILI.