Kati ya mwaka 2020 na 2022, mzozo kati ya chama cha Tigray People’s Liberation Front (TPLF) na serikali ya shirikisho ya Ethiopia ulisababisha vifo vya watu 600,000. Mashahidi wanane wa ukatili huu kwa hiyo wameamua kuwasilisha malalamiko nchini Ujerumani dhidi ya maafisa na maafisa wakuu wa Ethiopia na Eritrea kwa “uhalifu wa kivita” na “uhalifu dhidi ya ubinadamu.” Ya kwanza ya aina yake.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Malalamiko hayo yaliyowasilishwa mwezi Septemba 2024, na kuongezwa vipengele vipya mnamo Machi 20, 2025, yanahusu maafisa kumi na wawili wa ngazi za juu ambao majina yao hayajafichuliwa. Walalamikaji hao wanane ambao hawakutaka kutajwa majina yao na wengi wao wanaishi Ujerumani, walishuhudia matukio mbalimbali ya mauaji, ubakaji na watu kuwekwa kizuizini kiholela.
Hivyo kwa Nick Leddy, mwanasheria na mjumbe wa zamani wa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ambaye sasa ni mkuu wa idara ya madai ya chama cha Legal Action Worldwide, ambacho kiliandaa malalamiko hayo, kuna sababu nzuri za kuamini kwamba vitendo vilivyoripotiwa inajumuisha “uhalifu wa kivita” na “uhalifu dhidi ya ubinadamu.”
“Malalamiko hayo, ambayo yana takriban kurasa 100, yana uchanganuzi wa kina wa ushahidi wa chanzo wazi, pamoja na ushuhuda kutoka kwa wateja wetu ambao ni wahasiriwa, na ushuhuda kutoka kwa watu ambao walitupa muktadha. Ushahidi huu wote kwa pamoja unapaswa kutosha kwa mwendesha mashtaka wa Ujerumani kufungua uchunguzi na, kwa matumaini, kutoa hati ya kukamatwa.”
Mvutano mpya huko Tigray
Malalamiko yanakuja wakati hali ikizidi kuzorota tena katika jimbo la Tigray, huku kukiwa na mvutano kati ya Ethiopia na Eritrea.
Mnamo Machi 14, Umoja wa Afrika ulionyesha “wasiwasi wake mkubwa,” licha ya mawasilisho mengine dhidi ya taifa la Ethiopia yaliyowasilishwa mwaka 2022 na chama cha Nick Leddy mbele ya Tume ya Afrika ya Haki za Kibinadamu ambayo ilitoa, mnamo mwezi Oktoba 2022, hatua za dharura za kuzuia ukiukwaji huo kutokea tena.
