Gérald Darmanin azuru Rabat ili kuimarisha ushirikiano wa kimahakama kati ya Ufaransa na Morocco

Wakati ushirikiano wa kimahakama kati ya nchi hizo mbili ukiendelea kuimarika, hususan katika vita dhidi ya ulanguzi wa dawa za kulevya, Waziri wa Sheria wa Ufaransa, Gérald Darmanin, atakutana na mwenzake wa Morocco, Abdellatif Ouahbi, kujadili mapambano dhidi ya ugaidi na uhalifu uliopangwa.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Casablanca, François Hume-Ferkatadji

Katika ishara mpya ya kufufua uhusiano wa kidiplomasia unaloendelea kati ya Ufaransa na Morocco, Waziri wa Sheria wa Ufaransa, Gérald Darmanin, anatarajiwa mjini Rabat Jumapili Machi 9, ambako atakutana na mwenzake, Abdellatif Ouahbi. Katika mkutano wao, viongozi hao wawili wanatarajiwa kujadili hasa masuala ya mapambano dhidi ya ugaidi na uhalifu uliopangwa, katika muktadha wa kuimarisha ushirikiano wa mahakama kati ya nchi hizo mbili.

Katika wiki za hivi karibuni, hii imeangaziwa na matukio mawili muhimu. Mwishoni mwa mwezi wa Februari, washiriki wawili wanaodaiwa kuwa wa mfanyabiashara wa dawa za kulevya Mohamed Amra, aliyekabidhiwa hivi karibuni kwa mahakama ya Ufaransa baada ya kukamatwa huko Romania, walikamatwa huko Marrakech kwa ombi la Paris. Watu hao ambao wanashukiwa kushiriki katika maandalizi ya operesheni iliyomruhusu Mohamed Amra kutoroka kutoka kwa walinzi wake mnamo Mei 14 huko Normandy – tukio ambalo maafisa wawili wa magereza wa Ufaransa waliuawa – wote wawili wanaweza kurejeshwa Ufaransa hivi karibuni.

“Paka” arejeshwa Ufaransa

Mwezi wa Januari mwaka uliyopita, kwa upande mwingine, mtu aliyechukuliwa na Gérald Darmanin kama “mmoja wa walanguzi wakubwa wa dawa za kulevya nchini Ufaransa”, Félix Bingui anayejulikana kama “Paka”, alirejeshwa Ufaransa, miezi 10 baada ya kukamatwa kwake Morocco. Yeye ndiye anayedaiwa kuwa kiongozi wa kundi la Yoda, moja ya mashirika mawili ya Marseille ambayo yanatawala soko la dawa za kulevya.

Wakati wa mkutano wao, Gérald Darmanin na Abdellatif Ouahbi pia wanaweza kushughulikia suala la kutoa pasi za ubalozi, hati ambayo inaruhusu Ufaransa kuwafukuza wahamiaji haramu ambao hawana hati ya kusafiria. Mnamo mwezi wa Oktoba mwaka uliyopita, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa, Bruno Retailleau, alitangaza mjini Rabat kwamba makubaliano yamefikiwa kati ya Ufaransa na Morocco “kufupisha ukomo wa muda” wa kuwafukuza watu chini ya mkataab wa OQTF.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *