Gaza: Shirika la Ulinzi wa Raia latangaza kuuawa kwa 10 katika shambulio la Israeli

Shirika la Ulinzi la Raia la Palestina limetangaza vifo vya watu 10 wa familia moja katika shambulio la Israel lililotekelezwa usiku karibu na Khan Younis, kusini mwa Ukanda wa Gaza, usiku wa Alhamisi, Aprili 17, kuamkia Ijumaa, Aprili 18.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

“Timu zetu zimepata miili ya mashahidi 10 [watu waliouawa] pamoja na wengi waliojeruhiwa katika nyumba ya familia ya Baraka na nyumba zilizopembezoni zilizolengwa na vikosi vya Israeli vinavyokalia kwa mabavu katika eneo la Bani Suhaila, mashariki mwa Khan Younis,” Mahmoud Bassal, msemaji wa shirika hili la uokoaji, amesema kwenye Telegram.

Hayo yanajir wakati shirika la Ulinzi la Raia la Palestina lilitangaza siku ya Alhamisi, Aprili 17, kwamba mashambulizi ya anga ya Israeli dhidi ya mahema ya watu waliokimbia makazi yao yalisababisha vifo vya takriban watu 40 katika maeneo kadhaa katika Ukanda wa Gaza.

Gaza: Hamas inapinga makubaliano ya “sehemu” ya kumaliza vita (kiongozi)

Siku ya Alhamisi kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Kipalestina la Hamas lilisema linapinga makubaliano ya “sehemu” na Israeli kumaliza mapigano, na kukataa kabisa pendekezo la hivi karibuni la Israeli lililowasilishwa na mpatanishi wa Misri.

“Makubaliano hayo ya sehemu yanatumiwa na (Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin) Netanyahu na serikali yake kama  kuficha ajenda yake ya kisiasa (…) na hatutashiriki katika sera hii,” mpatanishi mkuu wa Hamas Khalil al-Hayya alisema katika hotuba yake ya televisheni, akiongeza kuwa kundi lake linataka “makubaliano kamili (…) badala ya kumaliza vita.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *